Tovuti rasmi ya serikali ya Marekani

ISIS Kanda Kubwa ya Sahara (ISIS-GS)

Afrika - Chini ya Jangwa la Sahara

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

ISIS Kanda Kubwa ya Sahara (ISIS-GS) ilianzishwa mnamo mwaka 2015 baada ya kujitenga kutoka al-Mourabitoun, kundi lililojitenga na al-Qa’ida, na kuapa utii kwa ISIS. Kimsingi likiwa na makao yake nchini Mali na likiendesha shughuli zake kwenye mpaka wa Mali na Nijeri, kundi hili pia lina harakati nchini Bukinafaso. ISIS-GS imedai kuhusika na mashambulio kadha, likiwemo lile la mnamo tarehe 4 mwezi Oktoba, mwaka 2017 dhidi ya doria ya pamoja kati ya Marekani na Nijeri kwenye eneo la Tongo Tongo, nchini Nijeri, ambalo lilisababisha vifo vya wanajeshi wanne wa Marekani na wanne wa Nijeri. Mnamo mwezi Novemba, mwaka 2019, ISIS-GS ilishambulia kambi ya jeshi la Mali na kuwaua wanajeshi 54.

Mnamo tarehe 23 mwezi Mei, mwaka 2018, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilitaja ISIS-GS kuwa Kundi la Kigaidi la Kigeni chini ya kifungu 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, kama ilivyorekebishwa. Hapo awali, mnamo tarehe 16 mwezi Mei, mwaka 2018, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje iliitaja ISIS-GS kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo yake ni kwamba, mali yote na maslahi ya ISIS-GS katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na ISIS-GS. Ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa ISIS-GS.

SUBMIT A TIP

Do Your Part. Secure a Safer World.

There are many ways to submit information to Rewards for Justice.

You may choose from multiple platforms and contact us in numerous languages. To process your information efficiently, we ask you to state your information as succinctly as possible, provide your name, location, and preferred language, and upload all relevant files such as photographs, videos, and documents to support your information. An RFJ representative will soon contact you. Please be patient, as RFJ reads every tip we receive.

Please visit our Tor-based tips-reporting channel at: he5dybnt7sr6cm32xt77pazmtm65flqy6irivtflruqfc5ep7eiodiad.onion

Wasilisha Kidokezi

Fanya Jukumu Lako - Dhamini Ulimwengu Salama Zaidi

Zipo njia nyingi kuwasilisha kidokezo.

Unaweza kuchagua kutoka majukwaa mengi na kuwasiliana nasi katika lugha nyingi.
Kuchakata taarifa yako kwa ufanisi, tunakuomba kusema taarifa zako kwa maneno mafupi na Dhahiri iwezekanavyo, kutoa jina lako, mahali uliko, na lugha unayopendelea, na kupakia faili zote husika kama vile picha, video, na hati kuunga mkono taarifa yako. Mwakilishi wa TKM atawasliana nawe hivi karibuni. Tafadhali uwe na Subira, kwa kuwa TKM husoma kila kidokezo tunachopokea.

Tafadhali tembelea idhaa yetu ya kuripotia vidokezo inayotumia mfumo wa TOR katika: he5dybnt7sr6cm32xt77pazmtm65flqy6irivtflruqfc5ep7eiodiad.onion

Skip to content