Tovuti rasmi ya serikali ya Marekani

Lashkar-e Tayyiba (LeT)

Asia Kusini na Kati

Fanya jukumu lako.

Kuhusu

Lashkar-e Tayyiba (LeT), ambayo pia inajulikana kama Jeshi la Waadilifu, ni kundi la kigaidi lenye makao yake nchini Pakistani ambalo lilianzishwa miaka ya themanini. LeT imetekeleza shughuli, yakiwamo mashambulio kadha ya ngazi za juu, dhidi ya majeshi ya India na shabaha za kiraia tangu mwaka 1993. Kundi hilo pia limeshambulia Majeshi ya Muungano nchini Afuganistani. LeT ilihusika na mashambulio ya kigaidi ya mnamo mwezi Novemba, mwaka 2008 jijini Mumbai, India, yaliyowaua watu 166 – wakiwamo raia sita wa Marekani – na kuwajeruhi wengine zaidi ya 300.

Mnamo tarehe 26 mwezi Disemba, mwaka 2001, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani ilitaja LeT kuwa Kundi la Kigaidi la Kigeni chini ya kifungu 219 cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, kama ilivyorekebishwa. Hapo awali, mnamo tarehe 20 mwezi Disemba, mwaka 2001, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ilitaja LeT kuwa Gaidi wa Kimataifa Mwenye Sifa Maalumu kuambatana na Amri ya Rais 13224, kama ilivyorekebishwa. Matokeo yake ni kwamba, mali yote na maslahi ya LeT katika mali, vyote vilivyoko chini ya mamlaka ya Marekani vimezuiwa, na watu wa Marekani kwa jumla wamekatazwa kushiriki kwenye miamala yoyote na LeT. Ni kosa la jinai kutoa kwa makusudi, au kujaribu au kula njama ya kutoa, msaada wa nyenzo au rasilimali kwa LeT.

SUBMIT A TIP

Do Your Part. Secure a Safer World.

There are many ways to submit information to Rewards for Justice.

You may choose from multiple platforms and contact us in numerous languages. To process your information efficiently, we ask you to state your information as succinctly as possible, provide your name, location, and preferred language, and upload all relevant files such as photographs, videos, and documents to support your information. An RFJ representative will soon contact you. Please be patient, as RFJ reads every tip we receive.

Please visit our Tor-based tips-reporting channel at: he5dybnt7sr6cm32xt77pazmtm65flqy6irivtflruqfc5ep7eiodiad.onion

Wasilisha Kidokezi

Fanya Jukumu Lako - Dhamini Ulimwengu Salama Zaidi

Zipo njia nyingi kuwasilisha kidokezo.

Unaweza kuchagua kutoka majukwaa mengi na kuwasiliana nasi katika lugha nyingi.
Kuchakata taarifa yako kwa ufanisi, tunakuomba kusema taarifa zako kwa maneno mafupi na Dhahiri iwezekanavyo, kutoa jina lako, mahali uliko, na lugha unayopendelea, na kupakia faili zote husika kama vile picha, video, na hati kuunga mkono taarifa yako. Mwakilishi wa TKM atawasliana nawe hivi karibuni. Tafadhali uwe na Subira, kwa kuwa TKM husoma kila kidokezo tunachopokea.

Tafadhali tembelea idhaa yetu ya kuripotia vidokezo inayotumia mfumo wa TOR katika: he5dybnt7sr6cm32xt77pazmtm65flqy6irivtflruqfc5ep7eiodiad.onion

Skip to content